SAYARI YA IJUMAA VENUS-ZUHURA
SAYARI YA IJUMAA
VENUS-ZUHURA
Sayari hii
iko Mbingu ya 3, Malaika wake anayeiangalia anaitwa Ann-yaill au Anael ambaye
kazi yake ni kufanya doria Mbinguni. Jini anayetawala siku hii anaitwa Al
abyadh au jina la utani anaitwa AbĂș Hassan Zoob’aa au Hagith.
Siku zake ni
Ijumaa na Jumatatu usiku na nyota zake ni Mizani na Ng’ombe. au wenye majina
yanayoanzia na G, S, B, N, Z
Sayari hii ni
nyeupe na yenye kung’aa nayo inatembelea kila nyota katika muda wa siku 27 na
inapitia kila sayari katika muda wa miezi 10. kwa maana ikikaa kwenye nyota
yako mambo yanayokutokea yatakuwa yanahusiana na Sayari hii kama
yalivyoainishwa hapa chini
Mafusho yake
‘Mustaka’ ambayo yako kama vijiwe vidogo vidogo vya rangi ya kijivu.
INAHUSIKA NA
NINI
Sayari hii
ya Venus au Zuhura inahusika na Muafaka, Urafiki, Uzuri wa moyo, Mapenzi,
Masikilizano, Mapatano, Tabia nzuri, Mambo ya muziki, Starehe, Michezo na kila
kitu chenye kufurahisha mwanamke.
FANYA
YAFUATAYO
Siku ya
Ijumaa ni siku nzuri ya kuoa, kuanza urafiki na mwanamke, kufanya tendo la
ndoa, kusafiri, kufanya biashara, kupenda, mambo yote ya raha utakayofanya katika
Siku hii ni mazuri na yenye baraka.
Leo uza
vipodozi, uza nguo, uza vyombo vya muziki, anza kujenga nyumba, tengeneza gari,
anza kupeleka watoto shule nk.
HAJA UTAPATA
AU HUPATI
Leo Ijumaa
ukiulizwa kama haja itapatikana , jibu kwamba ikiwa mwanzo wa siku Saa 12 hadi
Saa 6 haja itapatikana tena hakuna vingine.
Ikiwa ni
kati ya siku haja itapatikana baada ya uzito na taabu.
Ikiwa mwisho
wa siku haja haipatikani milele

Comments
Post a Comment