WATOTO WA NYOTA YA MAPACHA
WATOTO WA NYOTA
YA
MAPACHA
Watoto wa
Nyota ya Mapacha ni wale waliozaliwa kati ya Tarehe 22 Mei mpaka tarehe 21 Mei
Watoto wa
Nyota hii ni wachangamfu wanaopenda urafiki na ni rahisi sana kuwarubuni na
kufikiwa kwa mtu yoyote. Kwa lugha nyingine watoto hawa wanacheka na mtu yoyote
awe anamfahamu au asiyemfahamu. Wazazi wa watoto hawa mnatakiwa muwaelimishe
sana watoto wenu kwani kuna hatari wanaweza wakarubuniwa na kuchukuliwa na mtu
wasiyemfahamu.
Ni watoto
wenye nguvu na bidii na wanapenda kujishughulisha na wakati mwingine inabidi
uwalazimishe kulala.
Wazazi wa
mtoto mwenye Nyota hii wanatakiwa wampe moyo wa kuwa na msimamo na juhudi ili
mtoto huyu akamilishe malengo yake.
Watoto wa Nyota hii huwa wanapenda sana kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.anafanya jambo hili anaacha anafanya hili anaacha, matamano yao ni kama vile maji kupwa na maji kujaa.
Watoto wa Nyota hii huwa wanapenda sana kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.anafanya jambo hili anaacha anafanya hili anaacha, matamano yao ni kama vile maji kupwa na maji kujaa.
Ni vizuri
kwako wewe mzazi kumsistiza awe huru kuelezea jambo lake au anachokitaka.Watoto
wa Nyota hii watakubali kupewa adhabu au kunidhamishwa kama ikiwa kuna sababu
za kweli na umemuelezea akaelewa sababu ya wewe kumpa adhabu hiyo.
Tatizo kubwa
utakalolipata wewe mzazi ni kumkuta mtoto huyu akifanya jambo ambalo hulipendi
kwa sababu ni wajanja sana na hufanya mambo haraka haraka. Na ukimkamata
atakuwa na majuto sana na atahakikisha huwezi kumkata tena. Wazazi wengi
huwaona watoto hawa kama nusu malaika na nusu shetani.
Watoto hawa huwa wanapenda sana mijadala na kubishana na mwishowe hutokea ugomvi hasa na kaka zao au dada zao wale ambao yeye anawaona kama akili zao ni ndogo.
Watoto hawa huwa wanapenda sana mijadala na kubishana na mwishowe hutokea ugomvi hasa na kaka zao au dada zao wale ambao yeye anawaona kama akili zao ni ndogo.
Wanauwezo wa
kubadili maneno tena kwa uhakika mkubwa kiasi kwamba wewe mzazi ukashindwa
kujua kama anayosema ni ya ukweli ama anadanganya.

Comments
Post a Comment