Posts

SAYARI YA IJUMAA VENUS-ZUHURA

Image
SAYARI YA IJUMAA VENUS-ZUHURA Sayari hii iko Mbingu ya 3, Malaika wake anayeiangalia anaitwa Ann-yaill au Anael ambaye kazi yake ni kufanya doria Mbinguni. Jini anayetawala siku hii anaitwa Al abyadh au jina la utani anaitwa AbĂș Hassan Zoob’aa au Hagith. Siku zake ni Ijumaa na Jumatatu usiku na nyota zake ni Mizani na Ng’ombe. au wenye majina yanayoanzia na G, S, B, N, Z Sayari hii ni nyeupe na yenye kung’aa nayo inatembelea kila nyota katika muda wa siku 27 na inapitia kila sayari katika muda wa miezi 10. kwa maana ikikaa kwenye nyota yako mambo yanayokutokea yatakuwa yanahusiana na Sayari hii kama yalivyoainishwa hapa chini Mafusho yake ‘Mustaka’ ambayo yako kama vijiwe vidogo vidogo vya rangi ya kijivu. INAHUSIKA NA NINI Sayari hii ya Venus au Zuhura inahusika na Muafaka, Urafiki, Uzuri wa moyo, Mapenzi, Masikilizano, Mapatano, Tabia nzuri, Mambo ya muziki, Starehe, Michezo na kila kitu chenye kufurahisha mwanamke. FANYA YAFUATAYO Siku ya Ijumaa ni siku nzuri ya ...

SAYARI YA JUMATANO MERCURY-ATTARID

Image
SAYARI YA JUMATANO MERCURY-ATTARID Sayari hii iko Mbingu ya 2, Malaika wake Mikyaail au Raphael. Jini anayetawala Jumatano anaitwa Barkaan au Ophiel, Siku zake ni Jumatano na Jumamosi usiku na Nyota zake ni Mapacha na Mashuke au wenye herufi zinazoanzia C, O, F, R. Sayari hii ni ya kijani kibichi na wakati mwingine hugeuka wekundu, hupitia katika kila nyota siku ishirini na nane na kupitia katika kila Sayari kwa miezi sita. kwa maana ikikaa kwenye nyota yako mambo yanayokutokea yatakuwa yanahusiana na Sayari hii kama yalivyoainishwa hapa chini Dua ya kusoma siku ya Jumatano ni ‘Yaa ghaniyu’ yaa adhwim. Kafara ya Jumatano ni ‘Mchanga mwekundu unauusomea au kunuwia haja uitakayo au umwage mbele yako au umpige nayo adui yako na atapata matatizo. Mafusho yake yanaitwa Kashuu Muhlib au ‘kachiri’ ambayo yako kama maua yanayokauka na rangi yake ni kahawia ‘Brown’ INAHUSIKA NA NINI? Sayari hii ya Mercury-Attarid inahusika na mambo yanayohusiana na Adabu, Malezi mema, Mantik...

NYOTA ZENU SIKU NZURI NA MBAYA ZA KILA NYOTA:

Image
NYOTA ZENU SIKU NZURI NA MBAYA ZA KILA NYOTA: PUNDA: Majina ya kuanzia na herufi A, M, Y. Siku yao nzuri: Jumanne mchana Siku Mbaya: Jumanne usiku na Jumatano mchana Ni siku za Mikosi, Kifo, Kesi, na mabalaa, usifanye mapenzi, ni siku ya mikosi na balaa kwa watoto. NG’OMBE: Majina ya kuanzia na herufi B, N, Z. Siku yao nzuri: Ijumaa mchana Siku Mbaya: Jumamosi na Jumatano usiku Shida yoyote ikikufikia wakati huu haiponi au itakumaliza. MAPACHA: Majina ya kuanzia na herufi C, na O. Siku yao nzuri: Jumatano mchana Siku Mbaya: Jumanne usiku na Jumatatu mchana KAA: Majina ya kuanzia na herufi D au P. Siku yao nzuri: Jumatatu mchana Siku Mbaya: Jumanne mchana SIMBA: Majina ya kuanzia na herufi E na Q Siku yao nzuri: Jumapili Siku Mbaya: Alkhamisi mchana na Jumatatu mchana MASHUKE: Majina ya kuanzia na herufi F na R. yao nzuri: Jumatano mchana Siku Mbaya: Jumanne mchana MIZANI: Majina ya kuanzia na herufi G na S. Siku yao nzuri: Ijumaa mchana ...

TABIA ZA NYOTA KATIKA MAPENZI

Image
TABIA ZA NYOTA KATIKA MAPENZI PUNDA Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisia na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya kufanya chochote. “SASA HIVI” hayo ndio mambo wanayotaka kusikia. Ni watu wasiokuwa na subira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu, wakati wote wanajiona kwamba “Wanajua sana”. Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri, wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu NGOMBE Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka. Pamoja na kwamba asili yao ni...

JUA MAANA YA NAMBA YAKO YA SIMU

Image
JUA MAANA YA NAMBA YAKO YA SIMU Unapotaka kutafsiri namba yako ya simu tumia tarakimu nne za mwisho kwani hizi ndizo namba pekee ambazo ni tafauti na za watu wengine katika mtandao mmoja. Jumlisha tarakimu hizo nne hadi ufikie jumla ya tarakimu moja (single digit) yaani jumla iwe kati ya 1 na 9. JUMLA IKIWA 1 Hii ni namba yenye nguvu sana na ni namba ya kiume, ambayo inakuza nguvu zako binafsi ambayo inakuwezesha pia kuwashawshi watu wengine. Tahadhari usiwe mbabe kwa watu. Hii pia ni namba nzuri sana kwa biashara na kazi lakini sio namba nzuri ya aliye mpweke kumtafuta mpenzi. JUMLA IKIWA 2. Hii ni namba ya mapenzi, ni namba nzuri kwa walio wapweke kutafuta wapenzi. Namba hii inaashiria hisia, mawasiliano ya kibusara na ushirikiano, pia ni namba nzuri ya biashara ya huduma na sio nzuri kwa madalali na watu wabishi. JUMLA IKIWA 3 Namba hii inaashiria ubunifu, ucheshi, hii ni namba nzuri kwa wasanii, wanamziki na vijana. Namba hii haina muelekeo lakini ina mvuto na ni asi...

WATOTO WA NYOTA ZA MSHALE

Image
WATOTO WA NYOTA ZA MSHALE Nyota ya Mshale kwa watoto waliozaliwa kati ya Tarehe 23 November mpaka tarehe 21 Desemba Watoto wa Nyota hii wana tabasamu na bashasha ya hali ya juu, hata katika picha za pamoja nyumbani au shule au katika kikundi chochote itakuwa rahisi kwako kumtambua. Watoto hawa wanapenda sana matukio na wako tayari hata kwenda mbali kuyatafuta matukio hayo . wana tabia ya kupenda jambo Fulani moja kwa moja, kwa ni jukumu la wazazi wa Watoto hawa kuwafunza kuhusu ubaya na uzuri wa mambo hii itawasaidia katika kukuza kipaji chao cha asili cha kuona mbali Mzazi unatakiwa uwahimize sana wajishughulishe na mambo yote ya kutumia nguvu na akili. Watoto hawa huwa wanafurahia sana kufanya kazi za kawaida lakini huwa wanachoka haraka ni vizuri kwa mzazi ukitumia nafasi hii kuwafanya wajishughulishe na kazi ambazo zitakuwa na manufaa kwao hapo baadae. Pamoja na hayo Wanaweza kuwa wasumbufu na wenye kusita sita au kuchelewesha muda unapompa majukumu au kazi ambazo ha...

WATOTO WA NYOTA ZA MASHUKE

Image
WATOTO WA NYOTA ZA MASHUKE Nyota ya Mashuke kwa watoto waliozaliwa kati ya tarehe Tarehe 23 Agosti mpaka tarehe 23 Septemba. Watoto wa Nyota hii ni waangalifu, wenye jitihada, tegemezi, wakimya wa wana kipaji cha ajabu cha kuiga mambo. Ni watoto ambao wanaopenda sana unadhifu hasa wakiwa shule na wanatekeleza vizuri wajibu wao wakiwa shuleni. Hawaogopi majukumu ya darasani na huwa wanafanya vizuri sana katika mambo ya kuandika (Litreture) ni vizuri kuwasaidia katika mambo kama hayo. Hawa watoto hawa wana hisia kubwa lakini wana aibu sana na wanapenda sana usalama na mapenzi ya wazi kutoka kwa na wazazi wao. Wakihisi kuwa hawapati hayo wanayoyataka basi huwa hujifanya wanaumwa ingawa sio wagonjwa ili wabembelezwe na wapate wanachokitaka. Ni watoto wadadisi sana na anapotaka kujua jambo basi hutuma upole na lugha tamu na ya kistaarabu mpaka utamwambia analotaka kujua Wanapenda sana kujishughulisha, ukimskia anakwambia anaumwa na tumbo basi wewe usiangalie amekula nini wewe...