SAYARI YA JUMATANO MERCURY-ATTARID
SAYARI YA
JUMATANO MERCURY-ATTARID
Sayari hii
iko Mbingu ya 2, Malaika wake Mikyaail au Raphael. Jini anayetawala Jumatano
anaitwa Barkaan au Ophiel,
Siku zake ni
Jumatano na Jumamosi usiku na Nyota zake ni Mapacha na Mashuke au wenye herufi
zinazoanzia C, O, F, R.
Sayari hii
ni ya kijani kibichi na wakati mwingine hugeuka wekundu, hupitia katika kila
nyota siku ishirini na nane na kupitia katika kila Sayari kwa miezi sita. kwa
maana ikikaa kwenye nyota yako mambo yanayokutokea yatakuwa yanahusiana na
Sayari hii kama yalivyoainishwa hapa chini
Dua ya
kusoma siku ya Jumatano ni ‘Yaa ghaniyu’ yaa adhwim.
Kafara ya Jumatano
ni ‘Mchanga mwekundu unauusomea au kunuwia haja uitakayo au umwage mbele yako
au umpige nayo adui yako na atapata matatizo.
Mafusho yake
yanaitwa Kashuu Muhlib au ‘kachiri’ ambayo yako kama maua yanayokauka na rangi
yake ni kahawia ‘Brown’
INAHUSIKA NA
NINI?
Sayari hii
ya Mercury-Attarid inahusika na mambo yanayohusiana na Adabu, Malezi mema,
Mantiki, Kupata kitu, Fasihi ya lugha, Ufahamu, Uelewa, Elimu, Urafiki, Hila na
kudanganya, Hesabu, Vitabu, Sanaa za aina zote, Ukatibu au Ukarani, Shule au Kumpeleka
mtoto shule.
Vile vile
inahusiana na mambo ya Nakshi, masuala ya Urembo, kuandaa majeshi, nidhamu na
leo ni siku nzuri kuvaa nguo za hariri. Kwa ujumla ni Sayari ya mapato.
FANYA
YAFUATAYO
Siku ya
Jumatano ni siku nzuri ya kuwafukuza maadui au kuwapatanisha mke na mume,
wapenzi au Marafiki waliogombana au kama wewe ni kiongozi wa Nchi ni siku nzuri
kuanza kukusanya majeshi kwa ajili ya kupigana vita.
Siku ya leo
unashauriwa kuwa ujihadhari kuvaa nguo mpya unaweza kupata balaa, vilevile
unashauriwa usisafiri kwa sababu unaweza kupatwa na upepo mbaya.
Leo
Jihadhari sana kufanya Biashara hasa kununua na kuuza, Leo ni siku nzuri kwa
biashara ya nguo au udobi tu au biashara ya kufundisha watoto au wewe mwenyewe
kuanza masomo ya aina yeyote.
HAJA UTAPATA
AU HUPATI?
Jumatano
ukiulizwa kama haja itapatikana, jibu kwamba kama ni mwanzo wa siku kuanzia Saa
12 hadi Saa 5 haja haipatikani.
Katikati ya
siku kuanzia Saa 6 hadi Saa 9 haja au ushindi utapatikana kwa taabu na mashaka.
Jioni
kuanzia Saa 9 hadi Saa 12 haja itapatikana kwa urahisi.
SUALA LA
ANAEULIZA?
Mtu akikujia
siku ya leo atakuwa anataka kujua juu ya kitu chenye kuundwa undwa, chenye
thamani au ni kama pesa au kitabu au khatima au katibu mkuu au mjumbe au
mhasibu.
Jumatano
ukiulizwa kuhusu watu waliogombana au maadui waliokosana sema kwamba kati yao
wawili hamna kheri wala shari. Mwambie kwamba kila mtu kati yao anamfikiria
mwenzie ubaya na maovu, mwambie kwamba kati yao kuna fitina kubwa na hakuna
maelewano wala muafaka.
Ukiulizwa
kuhusu kilichopotea, sema kwamba kitu hicho hakipatikani mpaka zipite siku
nyingi ndio kitaonekana.
Jumatano
ukiulizwa juu ya mtu aliye mbali, sema kwamba mtu huyo atakuja hivi karibuni,
sasa hivi au leo au wakati wa Magharibi au siku yeyote kabla ya Jumatano.
Mwambie
kwamba yeye ni mzima na mali yake ni salama na hivi sasa yuko katika gari au
ndege au meli anakuja tokea sehemu za Magharibi na anaongozana na mtu
mashuhuri.
Pia mwambie
kwamba kuna kitu kidogo alichopoteza kama Pesa au Mnyama au Gari au kipandio
kuharibika na haitozidi siku tano au 10 atarejea.
Ukiulizwa
kuhusu mwaka huu utakuwaje, mwambie kwamba mwanzoni na mwishoni mwaka utakuwa
mbaya na vifo vitakuwa vingi vitakavyosababishwa na Subiani na atakufa msomi
mkubwa wa mji huo.
KHABARI
Leo Jumatano
Ukiulizwa juu ya khabari, sema kwamba khabari yeyote utakayopata leo ikiwa ni
mbaya au nzuri au ikiwa inahusu Mwanaume au Mwanamke au yasiyokuwa hayo basi
khabari hiyo ni kweli kabisa.
MAGONJWA
Jumatano
Ukiulizwa juu ya Mgonjwa, sema kwamba huyo Mgonjwa, ugonjwa wake unatokana na
upepo wenye kuweza kutibika. Mwambie kwamba ni ugonjwa wa kuchanganyika na
katika kichwa chake kuna kitu kichafu.
Mwambie
kwamba Mgonjwa huyo anaumwa mwili mzima na kuna kitu anahisi kinatembea kutoka
kitovuni mpaka mgotini. Mgonjwa ana maumivu makali katika shingo yake na
ugonjwa huu huwa unamrudia mara kwa mara.
Mwambie
mashahiba au watu wake wana wasiwasi kwamba atakufa kwa sababu ya maradhi hayo.
Mwambie
sababu ya maradhi hayo ni husda ya maadui zake na watu wengine ambao wanalitaja
jina lake usiku na mchana.
Mwambie dawa
yake ni yeye achinje hamani na aipike kwa samli ya Ng’ombe, aongeze kiini cha
yai na sukari kidogo na haba moja ya kufuri mchanganyiko huo apewe mgonjwa ale
atapata nafuu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
MWIZI
(MUHUSIKA)
Jumatano Ukiulizwa
juu ya (MUHUSIKA) Mwizi, sema kwamba ikiwa ni mwanzo wa siku Mwizi atakuwa ni
mtu mwenye rangi ya kahawia, mng’avu, mwenye pua ndefu na =mwenye haya kidogo.
Mwambie
kwamba (MUHUSIKA) Mwizi huyo ni msomi au mwenye kusomesha au msomaji ama yeye
anasomesha watoto wa watu. Sema ni mtu mwenye umbo fupi na atakuwa mtu wa
karibu yako mfano familia yako au rafiki yako au kipenzi chako au jirani yako.
Mweleze huyo Mwizi anapenda kubeba vitabu au vitu kama hivyo.
Mweleze kitu
kilichoibiwa kimetundikwa kwenye hewa au kimezikwa ardhini lakini kitapatikana.
Mwambie
ikiwa ni mwisho wa siku au jioni basi atakuwa mtu mwenye rangi nyekundu mwenye
umbo fupi na ana nywele nzuri. Mweleze kwamba kijana huyo ni msomi au ni mwenye
kuhifadhi Koran au Biblia.
Sema kwamba
kitu alichokiiba amebadilishana na kitu kingine. Mweleze huyo aliyebadilishana
nae ni mtu mzuri, tajiri na ni kijana wa kiume wa hapo mjini.
Mwambie kitu
kilichoibiwa hakitaonekana ila kwa taabu na shida.
SAFARI
]Jumatano
Ukiulizwa juu ya Safari, sema kwamba kama ni safari ya nchi kavu basi itatimia,
lakini ikiwa ni safari ya baharini au nchi za nje itabidi ungoje kwa muda wa
wiki mbili au miezi miwili au miaka miwili.
Endelea
kumweleza kwamba kuna uzito na taabu hasa kwa vile hivi sasa unashirikiana
katika safari hiyo na mtu mmoja ambaye ni Muongo au kuna mtu mnaushirika juu ya
jambo au kuchanganyika pamoja.
Mwambie
kwamba ajihadhari naye kwani mtu huyo ni mwongo na atakushughulisha katika
mambo mengi ya uongo kuhusu safari hiyo.
Mweleze
kwamba akisafiri baharini bila kungoja hizo wiki mbili atapigwa na upepo mkali
na meli au chombo atakachosafiria kitazama au kupinduka lakini yeye
atanusurika.
Mwambie
kwamba habari hizo inahusu safari inayoanzia mwanzo wa siku lakini kama
akisafiri katikati ya siku kuna mawili yatatokea, kuna uzito na kuna wepesi.
Mwambie
mwanzo wa siku ni kwa safari za nchi kavu tu, kwa safari za baharini lazima
asubiri wiki moja au mwezi mmoja au miaka miwili.
NDOA
Leo Jumatano
Ukiulizwa juu ya Ndoa sema kwamba ndoa itawezekana tu ikiwa ni kwa mjane ambae
si mtu wa kwenu au ifungwe mbali na hapo.
Sema kwamba
Mwanamke anayetaka kuolewa hana mapenzi ya dhati kama alivyo mwanamme na lazima
ifanyike dawa kurekebisha mapenzi ya Mwanamke.
Mweleze
kwamba mazungumzo ya ndoa yapo na yatakuwepo lakini kuna mtu wa nje ambaye
anayefanya mipango hiyo ya Ndoa mpaka akirudi ndio ndoa itatimia.
Kwa kawaida
Jumatano ndoa huwa haitimii kwa sababu mwanamke huwa anapata ushawishi kutoka
kwa mwanamme mwingine ambaye hayupo hapo, yupo mbali. Ukitaka ndoa muone mwalimu
akufanyie azima ndipo ndoa itatimia inshallah.
MIMBA
Leo Jumatano
Ukiulizwa juu ya Mimba sema kwamba mzazi atazaa watoto wawili (Mapacha), Mke na
Mume. Mweleze kwamba mmoja ya watoto hao ana damu ya Jini na mwingine ana damu
ya Kibinaadamu.
Mweleze kwamba
mtoto wa kiume atakuwa mtambuzi na mwenye akili nyingi, msomi na atakuwa na
umri mrefu na utajiri mwingi na mtoto huyo atapendwa na wengi kwao na nje ya
nchi.
NANI MSHINDI
Ukiulizwa
leo Jumatano nani atashinda sema kwamba kwa wanaoshindana matokeo ni sare
hakuna mshindi wala mshindwa.
Sema kwamba kila mmoja amefanya njama mbaya kwa mwingine na kuna
fitina mbaya kati yao na mwisho hawatakubaliana wala kusikilizana.

Comments
Post a Comment