TABIA ZA NYOTA KATIKA MAPENZI
TABIA ZA NYOTA
KATIKA MAPENZI
PUNDA
Punda ni
wakali na wachangamfu, wenye hisia na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya
kufanya chochote. “SASA HIVI” hayo ndio mambo wanayotaka kusikia.
Ni watu
wasiokuwa na subira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Ni
viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu, wakati wote wanajiona
kwamba “Wanajua sana”.
Kwa ujumla
wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi
kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu
wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia
katika mapenzi bila kufikiri, wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi
kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu
ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu
NGOMBE
Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.
Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.
Pamoja na
kwamba asili yao ni udongo, wanaweza kuwa ni wenye mahaba na mapenzi makubwa
kwa wapenzi wao.
Uhakika wa
mapenzi ndio jambo kubwa ambalo wenye nyota hii huangalia kwanza na baadae
Penzi hilo liwe lenye hisia na mpangilio.
Pamoja na
hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu
wenye shauku kutovutiwa nao.
Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.
Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.
Wanachotakiwa
kufanya ni kujitahidi kuwapa nafasi wapenzi wao la sivyo watajikuta wako peke
yao. Ndoa kwao ndio uamuzi mzuri kuliko kuishi na wapenzi. Tabia yao ni ya
kudumisha jambo fulani wanaloliamini au walilolianzisha na hawapendi
kubadilishwa.
3.MAPACHA
Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na
kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu
wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi
wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda
mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano
unazidi kuwepo.
Katika
mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa
wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia
hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
KAA
Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa wenye nyota hii pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanapenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.
Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa wenye nyota hii pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanapenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.
Wanapenda
sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao
hakuna mapenzi ya nusu nusu na wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae
milele.
Wenye Nyota
hii bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha hivyo
basi huwa hawana raha.
Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.
Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.
Ni wagumu
sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi wako radhi wao waumie
kuliko kuachana na anayempenda.
SIMBA
Tabia ya Simba ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanao wapenda.
Tabia ya Simba ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanao wapenda.
Furaha haina
mpaka katika mapenzi ya simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza
dhahiri wanapompenda mtu.
Baada ya
hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza. Wao wanathamini sana mapenzi na juu
ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu
wapenzi wao.
Wanapenda
kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua
vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Kwa nje
wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa
wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata
hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.
MASHUKE
Pamoja na kwamba wanaonekana ni watu wenye aibu kwa undani na kujiamini, wenye nyota hii hupumzika na kunawiri wanapokuwa katika mapenzi.
Pamoja na kwamba wanaonekana ni watu wenye aibu kwa undani na kujiamini, wenye nyota hii hupumzika na kunawiri wanapokuwa katika mapenzi.
Ni watu
ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya
kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi
lenyewe.
Wanapotafuta
mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani. Ni
vizuri kufikiria mara mbili kabla hujajiingiza katika mapenzi na Mashuke.
Inawawia
vigumu wao kukuanza wewe kimapenzi kwa sababu wana uhakika kwamba watashindwa.
Kinachowasaidia
ni subira na kuwaelewa wapenzi wao ndio maana mapenzi yanakua.
Mara
wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha
mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza.
Hata hivyo
wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa ya mpenzi
wake ili amshutumu.
Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao.
Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao.
MIZANI
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.

Watu wa
mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda
sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu
hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina matatizo na
zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii
wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala
la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana kumpendeza
mwanamke kwa maneneo matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo
kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla
wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao
waishi katika hali nzuri.
NGE
Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi
au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa
kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri. Inashauriwa wale wenye moyo mdogo
wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao
hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu
wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na
wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.
Ni watu
wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata
wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
MSHALE
Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.
Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.
Wenye nyota
hii wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa
kuwa na wapenzi wao. Ni watu wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya
kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.
Wanapoingia
katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha.
Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa
sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao
wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa
na kutokuwa na uhuru.
Ni watu
wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali na inashauriwa
kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa
taabu.
MBUZI
Watu wenye nyota hii wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi.

wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana
katika kuchagua wapenzi.
Jambo
jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa
kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.
Kwa ujumla
ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa
wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao
katika mapenzi ni usalama.
NDOO
Wenye nyota ya Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.

Wako tayari
kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa
katika mambo binafsi. Niwa watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na
wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.
Mara nyingi
inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa
waaminifu.
Ni watu
ambao wenye kusema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi
wao.
Katika ngono
kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na
hawakubali kuingiliwa.
Wakati
mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya
wapenzi wao washindwe kuwaelewa.
SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
Wenye nyota ya Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
Kuwa katika
mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa
wapenzi wao wana huruma nyingi.
Ni watu
wenye hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.
Mara nyingi
huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango
yao ya baadaye.
Ni watu
wenye kuyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama
binaadamu wasio wa kawaida.
Tatizo lao
kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo
au firika za kimapenzi ambazo hazipo katika dunia hii.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa
wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapenzi wao waishi kiroho.
Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yasipotimia huwa wanavunjika moyo

Comments
Post a Comment