JE MAJINI WANAWEZA KUTUMIKA?
JE MAJINI
WANAWEZA KUTUMIKA?
Majini
wanaweza kutumika kwa kazi mbalimbali ambazo Binadamu anaweza kumtuma.
Mwenyezi Mungu aliwaamuru Majini wamtumikie Mfalme Suleimani na wakawa wanamfanyia Kazi kadri anavyotaka yeye.
Mwenyezi Mungu aliwaamuru Majini wamtumikie Mfalme Suleimani na wakawa wanamfanyia Kazi kadri anavyotaka yeye.
Katika
Biblia 1 Wafalme 5: (13-17).
Biblia
inaeleza jinsi nyumba ya Suleimani ilivyokuwa ikijengwa kimya kimya. ... “Na
nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwishachongwa chimboni,
wala nyundo wala shoka, wala chombo cha chuma chochote sauti yake haikusikika
ilipokuwa ikijengwa Nyumba”.
Majini
vilevile wanatumiwa na watu katika kupata habari za mambo mbalimbali kwa sababu
wao wana uwezo wa kupata habari angani.
Majini
vilevile wanatumika katika ulinzi wa kulinda majumba au kulinda watu au
Mikutano au Shughuli yeyote na vilevile wanaweza kutumika katika vita.
Wao wanajigeuza katika maumbo aidha ya Binaadamu au Mnyama na kushiriki katika vita.
Wao wanajigeuza katika maumbo aidha ya Binaadamu au Mnyama na kushiriki katika vita.
Mfano
Shetani mmoja alijigeuza kwa mfano wa Binaadamu mmoja aitwae Saraqa Bin Malik
na kushiriki vita vya Badri na kuwaahidi Makafiri ushindi mkubwa lakini
alipoona Majeshi mawili ya Malaika wanateremka kutoka Mbinguni alitimka na
kutoroka.
JE TUNAWEZA
KUJIKINGA NA MASHETANI?
Zipo njia
nyingi za kujikinga na Mashetani lakini kubwa zaidi ni kutumia Jina la Mwenyezi
Mungu na kumtaka Mungu akuepushe na Shetani mbaya Naye atakusaidia.
Shetani ana
Maudhi mengi sana kwa Binadamu kwa sababu anapenda kujishirikisha na Binadamu
katika kila kitu kama vile katika kula, kunywa, kufanya Mapenzi, kutembea,
Kuishi ndani ya Nyumba na hupenda kufanya hayo yote pale Mwanadamu anapopotea
na kumsahau Mwenyezi Mungu.
Shetani
vilevile anamgusa kila Mtoto anayezaliwa katika dunia hii. Mtoto ambaye
hajaguswa na Shetani ni Yesu au Issa Bin Maryam hayo ni kwa mujibu wa maelezo
ya Qurani na Mtume Muhammad (SAW).
Mashetani
vilevile ndio wanasababisha Ugonjwa wa Tauni (Plague – Ugonjwa unaoambukiza).
Mtume Muhammad (SAW) ameeleza “Hakika kuangamia kwa Umma wangu kunatokana na
kushuka Hadhi yao na Ugonjwa wa Tauni na Adui yenu Mkubwa anatokana na Jini, na
Hiyo kwenu ni Shahada”.
Hivyo basi
ili kujiepusha na maovu ya Shetani unashauriwa kumweka mbele Mwenyeezi Mungu
katika lolote unalolifanya ukiwa Nyumbani au popote pale.
Haya ni
baadhi ya maelezo kuhusu Majini, zidi kutembelea tovuti hii mara kwa mara kwani
hii ni mwanzo tu na tutazidi kuwaletea habari za ndani kuhusu majini na tabia
zao, jinsi ya kujikinga nao au kushirikiana nao.
Marafiki na
Maadui wa Majini
MARAFIKI WA
MAJINI:
Majini huwa
wanafanya Urafiki na Binadamu lakini Marafiki wao wakubwa ni Ngamia.
Baadhi yao wanaishi katika nyumba tunazoishi na ukitaka kuwafukuza unasoma Quran au Biblia au kumtaja Mwenyezi Mungu.
Baadhi yao wanaishi katika nyumba tunazoishi na ukitaka kuwafukuza unasoma Quran au Biblia au kumtaja Mwenyezi Mungu.
Majini hukusanyika
na kuongezeka giza linapoingia au unapopatwa Mwezi, na huwa wanakimbia
wanaposikia Adhana au Kengele ya kamba.
Majini wengi wanapenda kukaa baina ya kivuli na jua na siyo vizuri kukaa eneo hilo.
Majini wengi wanapenda kukaa baina ya kivuli na jua na siyo vizuri kukaa eneo hilo.

Comments
Post a Comment